Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya amesema Mfumo wa utoaji taarifa za biashara nchini utasaidia kupunguza vishoka na kuongeza uwazi na uwajibikaji katika utoaji wa huduma kwa taasisi za umma.
Akizungumza na wadau wa biashara leo Septemba 30,2019, Manyanya amesema mfumo huo ukitumiwa vizuri utaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya biashara nchini.
Amesema mfumo huo utasaidia wafanyabishara kujua hatua kwa hatua namna ya kupata kibali cha biashara anapotaka kupeleka bidhaa zake nje ya nchi, kuingiza na kuzipitisha nchini.
Manyanya amesema utekelezaji wa mfumo huo ni hatua kubwa kwa nchi katika kutimiza makubaliano ya utekelezaji wa kipengele cha Mkataba wa Uwezeshaji Biashara nchini ya Shirika la Biashara Duniani (WTO) ulioanza kutekelezwa Februari 2017.
"Kwa ujumla mfumo huu utaboresha mazingira ya biashara nchini hivyo, kuchangia uchumi wa nchi kukua kwa sababu biashara zitakua na uzalishaji kuongezeka kutokana na urahisi wa upatikanaji wa taarifa za masoko ya nje," amesema Manyanya.
Ameeleza kuwa pamoja na mfumo huo, serikali imeendelea na jitihada mbalimbali za kuboresha mazingira ya biashara nchini ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Pia amesema jitihada hizo zinajumuisha mipango mbalimbali ya maboresho iliyoanza mwaka 2000 ambayo inajumuisha Mpango wa Maboresho kwenye Mfumo wa Udhibiti wa biashara Tanzania ulioridhiwa Mei 2018.
Amesema tayari wizara na taasisi za serikali zimeanza kufanya maboresho katika maeneo ambayo ni rahisi kutrkelezwa bila kufanya mabadiliko ya sheria na matokeo yake yameanza kuonekana ndani ya muda mfupi.
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara (Brela), Andrew Mkapa amesema mfumo huo unafaida nyingi kwa mfanyabiashara kujua anapataje kibali au leseni mbalimbali kwa njia ya kielektroniki.
Amesema taarifa za taasisi zote na vibali zitawekwa kwenye mfumo huo wa tovuti hivyo, mfanyabiashara anaweza kuomba vibali bila kuzunguuka.
Ameeleza kuwa mfumo huo pia unapunguza gharama kwa wafanyabiashara ambao wanahitaji kuingiza, kusafirisha au kupitisha biashara mbalimbali.
"Tunategemea kuchukua maoni kwa watu wengi zaidi ili kuboresha mfumo huo uweze kuwa na manufaa hivyo, mpaka Desemba mwaka huu tutakuwa tumepata maoni kwa wadau wengi na tutazindua awamu ya kwanza," amesema Mkapa.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stellah Manyanya akizungumza katika mkutano wa wadau kuhusu mfumo wa utoaji wa taarifa za kibiashara nchini (Trade information Module), uliofanyika leo Septemba 30,2019 jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Afisa Mtendaji, Wakala wa Usajili wa Biashara (Brela) na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya maendeleo Biashara Tanzania (Tantrade).
Baadhi ya wadau mbali mbali wa mfumo wa utoaji taarifa za kibiashara nchini, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stellah Manyanya (hayupo pichani) katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.