-->

Anaandika Abdullatif  Yunus - Michuzi TV
Serikali Mkoani Kagera kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), wameendelea kuboresha mazingira wezeshi na rafiki kwa Mkulima katika Sekta ya Kilimo, hususani Mkulima wa zao la kahawa, ili kulifanya zao hilo kuwa na Tija kwa Mkulima na kujipatia faida.

Akibainisha Mabadiliko hayo ya Mfano Mkurugenzi wa TADB, Japhet Justine amesema Ndani ya Miaka miwili Benki imekuwa ikitoa mikopo kwa Vyama Vikuu vya Ushirika ikiwemo KDCU, KCU na Ngara  ili kumsaidia Mkulima wa Kahawa kupata pesa yake kwa haraka na uhakika, jambo ambalo limesaidia kupunguza magendo ya kahawa kwa kiasi kikubwa, kwani Mkulima ana uhakika wa kuuza kahawa yake katika chama chake cha msingi, na hivyo suala la magendo na kuuza kahawa changa maarufu kama (obutula) halina nafasi.

Kutokana na hali hiyo TADB wataendelea kutoa mikopo kwa vyama hivyo ili kumfanya Mkulima wa zao la kahawa kupata pesa yake ndani ya siku saba Mara baada ya kukusanya kahawa yake katika chama cha msingi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brig. Jen. Marco Gaguti awali akitoa salaam zake kwa wakulima Wilaayani Karagwe alipofika hapo kutaka kufahamu kama Kuna changamoto zinazowakabili wakulima hao, Mkuu huyo amethibitisha kuwa kwa sasa suala la kahawa sio tatizo kabisa, kuanzia malipo mpaka udhibiti wake juu ya magendo ya kahawa, hivyo anaweza kulala na kupata usingizi huku akifikiria mambo mengine na sio kahawa.

Aidha Mkuu wa Mkoa Kagera ameendelea kusisitiza na kupiga marufuku suala la Baadhi ya wanunuzi wa kahawa wanaonunua kahawa kinyemela kwa Ujanja, kuwa jambo hilo halitakiwi na Serikali haitosita kuchukua hatua kwa wtakaobainika kufanya hivyo.

Hayo yanajili wakati ambapo Oktoba Mosi ni Siku ya unywaji Kahawa Duniani, wakati maadhimisho haya Kitaifa yakifanyika Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera, ambapao siku hii ilianza kuadhimishwa rasmi Oktoba Mosi 2015.
 Mkuu wa Mkoa Kagera Brig. Jen.  Marco Gaguti akitoa salaam zake alipofanya ziara wilayani Karagwe na kuzungumza na wakulima kutaka fahamu changamoto zinazowakabili.

 Mkurugenzi mtendaji wa TADB Ndg. Japhet Justine akizungumza na wakulima Wilayani Kyerwa, katika ziara yake aliyoifanya  ili kuboresha hali za wakulima wa kahawa katika wilaya hiyo mkoani Kagera.