-->


Kampuni ya Tigo ambayo kwa sasa ni namba mbili kwa ukubwa hapa nchini.Kwa mujibu wa takwimu za TCRA Tigo ina wateja wapatao 11.6 Milioni.

Kampuni hiyo ni moja ya waanzilishi wa teknolojia ya intaneti yenye viwango vya kimataifa kupitia mtandao wa 2G na 3G.Aidha, imekuwa ya kwanza kuanzisha intaneti yenye kasi ya 4G-LTE na kuiboresha kwenda 4G+, jambo ambalo limedhihirisha utayari wake katika kuleta mapinduzi ya kidigitali hapa nchini.

Kwa mujibu wa Afisa Biashara Mkuu wa Tigo, Bw.Tarik Boudiaf, safari ya Tigo katika kuleta suluhu kidigitali kwa wateja wake ilianza baada ya Kampuni hiyo kufanya mageuzi ya kiuendeshaji na kuifanya kuwa kampuni ya kidigitali ikitoa bidhaa mbalimbali pamoja na intaneti ya kasi mbali na huduma za kawaida za kupiga simu, kutuma meseji na huduma za kifedha.

Kupitia dhamira yake ya kuleta mapinduzi ya kidigitali nchini, Tigo inakuwa mmoja wa kampuni za juu zenye kuchochea ueneaji na matumizi ya intaneti kwa wateja wake.

Aidha, kupitia mkakati maalumu, Tigo imeanzisha jitihada mbalimbali ambazo zimebadilisha mwenendo wa soko huku ikichangia katika agenda ya ujumuishwaji wa watu kidigitali nchini.

“Mkakati wetu ni kuendelea kuleta ujumuishwaji wa kidigitali na kuboresha mfumo wa maisha Tanzania.Tigo ni kampuni ya kwanza kuanzisha intaneti ya 4G na hivi karibuni imeleta teknolojia ya 4G+ iliyozinduliwa chini ya kampeni ya “Always a step ahead”. Hii inadhihirisha nia yetu ya dhati ya kuwaunganisha watanzania na intaneti ya kasi na ya uhakika huku tukiwajengea uelewa juu ya faida za huduma hii ya mtandao,” anasema Boudiaf.

Anaongeza “Tunatambua kwamba wateja wetu wanahitaji huduma ya uhakika na yenye ufanisi ambayo inahusisha teknolojia yenye miundombinu ya hali ya juu, vifurushi mahsusi pamoja na simu janja (smartphones) za kisasa pamoja na kuwapa maudhui yenye uhaisia”.

Ili kufanikisha malengo hayo, Afisa huyo anaeleza mikakati mbalimbali ya kuwezesha ueneaji wa intaneti ikiwamo uwekezaji mkubwa uliofanywa na Tigo kwenye ujenzi wa miundombinu ya teknolojia ya intaneti ya 4G ambayo imeboreshwa na kuwa 4G+ na hatimaye kukidhi mahitaji ya huduma za mtandao.

Aidha hatua hii sit u imeboresha huduma za kampuni hiyo bali imewezesha kukuza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Takwimu za Taasisi ya Kimataifa ya GSMA kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ya mwaka 2019, inaonyesha kuwa matumizi ya simu janja yataongezeka mara mbili ifikapo mwaka 2025 huku ukanda wa Afrika Mashariki ukitajwa kushuhudia ongezeko kubwa Zaidi.Ripoti inazitaja nchi za Rwanda na Tanzania kuongoza kwenye ukuaji huo.

Kadhalika,kutokana na ukweli kuwa matumizi ya mtandao hufanyika hasa kupitia simu za mkononi hivyo upatikanaji wa simu za bei nafuu ni chachu katika kuchochea ueneaji wa intaneti nchini. Katika hili, Boudiaf anasema “Tigo imetengeneza mkakati madhubuti wa kuchochea matumizi ya smartphones kwa watu nchini.Tunaamini kuwa kupitia kuingia ubia na wazalishaji wa simu za mkononi kama Kampuni ya Samsung, Tecno, Nokia, Infinix na Itel imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za simu na kuzifanya zipatikane kwa urahisi hadi kwa watu wenye kipato cha chini.”

Sambamba na hilo, Tigo imekuwa ikiendesha kampeni mbalimbali zenye lengo la kutoa simu kwa wateja ikiwamo ile ya Wagiftishe na hivi karibuni imekuja na kampeni ya Lamba Dume ambapo mbali na kutoa simu, zinatoa fursa ya kupata intaneti ya bure inayodumu kwa takribani mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa Afisa huyo, ijapokuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye tozo ndogo za intaneti kwenye ukanda huo, suala la kutengeneza vifurushi nafuu vya intaneti ni jambo la msingi. Mfano; Kifurushi cha Saizi Yako ni moja ya vifurushi ambavyo vinavyolenga kumpa mteja huduma ya intaneti bila mipaka ambapo mteja anaweza kujipatia intaneti kulingana na mahitaji yake.

Vilevile, upatikanaji wa maudhui ya ndani ni moja ya sababu za kuongeza matumizi ya intaneti.Tigo inatoa vifurushi mbalimbali ambavyo vinaruhusu wateja kujipatia maudhui yenye kukidhi mahitaji ambapo kupitia mtandao wa You Tube, StarTimes na DSTV wateja wanaweza kuunganishwa na chaneli hizo na kufurahia maudhui yenye uhalisia wa ndani.

Kuhusu suala la uridhishwaji wa huduma za mtandao zinazotolewa na Kampuni hiyo, Boudiaf anasema “Kupitia kufanya vumbuzi mbalimbali, Tigo inalenga kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora na zenye viwango kupitia bidhaa na huduma za kisasa kila wanapokutana na nembo yetu.Uwekezaji wa Tigo kwenye intaneti ya 4G umehakikisha kupatikana kwa intaneti ya uhakika na yenye viwango stahiki, nia hii ya Tigo inaiweka sekta ya mawasiliano kwenye viwango vya juu na kuleta mageuzi ya kidigitali,” .

Tigo Tanzania inajinasibu kwa kuongoza soko katika kuchochea maendeleo ya digitali na zaidi katika kuleta huduma zenye kukidhi mahitaji ya wateja na hii imesabisha kutengeneza huduma na bidhaa zenye kukidhi mahitaji ya soko soko la Tanzania.

Wateja wa Tigo wanafikiwa kote nchini kupitia njia mbalimbali ikiwamo maduka ya Tigo,dawati la huduma kwa wateja pamoja na mitandao ya kijamii ikiwamo Facebook, Twitter, WhatsApp na Instagram ambayo inampa fursa mteja kushiriki katika uboreshaji wa huduma kwa kutoa maoni juu ya huduma zitolewazo na kampuni hiyo.

Hatahivyo, fursa ya kuwaunganisha watanzania na huduma ya intaneti ya uhakika bado inatakiwa kupewa kipaumbele kutokana na ukweli kuwa bado idadi kubwa ya watu wanakaa nje ya mtandao (offline).