-->


Na Editha Karlo wa Michuzi Tv,Geita

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) umeibuka kuwa mshindi wa kwanza katika kundi la Bima na Hifadhi ya Jamii kwenye kilele cha maonyesho ya pili ya teknolojia ya uchimbaji na uwekezaji kwenye sekta ya madini.

Wakati wa sherehe za kufunga maonesho hayo kwenye viwanja vya CCM kalangalala mjini Geita ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Madini Mh. Dotto Biteko 

Mfuko wa bima ya afya unashukuru kwa kupata ushindi huu,kwani umetokana na ubunifu waliokuwa nao katika banda lao.

" Ushindi wetu umetokana na ubunifu wetu wa huduma tulizokuwa nazo kwenye banda letu vile vile sababu nyingine ni hali ya kufanya kazi kwa pamoja na kuthamini wateja waliofika kwenye banda letu kwaajili ya kupata huduma mbalimbali na kuwahudumia kwa umahiri na kuwajali"Alisema Meneja wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Mkoa wa Geita Elias Odhiambo

Odhiambo alisema kwa ujumla banda lao lilibeba "philosophy" ya utendaji kazi wa NHIF.Alisema Zaidi ya wananchi 1200 wametembelea katika banda lao huku wananchi 1080 wamefanya upimaji wa afya zao.

Baadhi ya wananchi waliofika katika banda la NHIF wamesema kuwa wamefurahishwa na huduma zilizokuwa zinatolewa kwa kipindi chote cha maonyesho."Mimi nilifika kwenye banda la mfuko wa bima ya afya nikapata huduma ya kupima macho bure,na wakanishauri wamefanya jambo zuri sana naomba waendelee na huu utaratibu siyo hadi wasubirie maonyesho"Alisema Kabula Mathias Mkazi wa Geita mjini

Maonesho ya Pili ya Uzalishaji na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yalifunguliwa rasmi tarehe 22/9/2019 na kufungwa tarehe 29/9/2019
Watumishi wa mfuko wa bima ya afya (NHIF)Mkoa wa Geita wakifurahia kombe la ushindi baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika kundi la Bima na Mifuko ya Hifadhi ya jamii kwenye kilele cha maonyesho ya pili ya teknolojia ya uchimbaji na uwekezaji kwenye sekta ya madini.
Baadhi ya watumishi wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuibuka mshindi wa jumla